Terms of Service — Gochati
Masharti ya matumizi ya huduma za Gochati
Kwa kuunda akaunti au kutumia Gochati, unakubali masharti haya. Tafadhali yasome kabla ya kuendelea.
1. Huduma ya Gochati
Gochati ni jukwaa la mawasiliano ya mtandaoni linalowaunganisha watumiaji kwa mazungumzo. Watumiaji wanawajibika kutumia huduma kwa heshima na kwa mujibu wa sheria zinazotumika.
2. Akaunti na taarifa
Toa taarifa sahihi wakati wa usajili, linda nenosiri lako na usimruhusu mtu mwingine kutumia akaunti yako. Una jukumu la shughuli zinazofanyika kupitia akaunti yako.
3. Umri na usalama
Ni lazima uwe na umri unaoruhusiwa kisheria kutumia huduma hizi. Hairuhusiwi kutumia Gochati kwa udanganyifu, vitisho, unyanyasaji, ulaghai, maudhui haramu au kuomba taarifa binafsi za wengine kwa njia isiyo salama.
4. Malipo, salio na ada
Akaunti inakuwa active moja kwa moja baada ya usajili. Kuboresha akaunti kunaweza kuhitaji malipo. Kiasi na masharti husika yataonyeshwa kwenye ukurasa wa malipo.
5. Matumizi yaliyokatazwa
Usitumie huduma kuwasilisha taarifa za uongo, kuingilia mifumo, kujaribu kupata akaunti za watu wengine, kutuma barua taka au kuendesha shughuli zisizo halali. Gochati inaweza kuzuia au kusimamisha akaunti inayokiuka masharti haya.
6. Faragha
Taarifa za akaunti hutumika kuendesha huduma, kuthibitisha malipo, kuzuia udanganyifu na kutoa msaada. Usitume taarifa za siri za malipo au nywila kwa watu wengine.
7. Upatikanaji na mabadiliko
Huduma inaweza kusitishwa kwa muda kwa ajili ya matengenezo, usalama au sababu za kiufundi. Gochati inaweza kusasisha masharti haya; toleo jipya litawekwa kwenye ukurasa huu.
8. Mawasiliano
Kwa msaada kuhusu akaunti au huduma, tumia njia ya Customer Service inayoonyeshwa kwenye Gochati.